Header Ads

Genk yaibuka na ushindi dhidi ya Athletic Bilbao, Samatta akitimiza dakika 126

Usiku wa October 20 2016 klabu ya KRC Genk inayochezewa na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Mbwana Samatta ilishuka katika uwanja wake wa Luminus Arena kucheza  mchezo wake wa tatu wa Europa League dhidi ya Athletic Bilbao ya Hispania.
1332726718_b9710027062z-1_20161020231728_000_g867rcd62-3-0
KRC Genk ambao tayari walikuwa wanaongoza msimamo wa Kundi F kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa, wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-0, magoli ya Genk yakifungwa na Jakub Brabec dakika ya 40 na Wilfred Ndindi dakika ya 83.
belgaimage-97252109
Nahodha wa Tanzania Mbwana Samatta aliingia dakika ya 56 kuchukua nafasi ya nahodha wao Thomas Buffel, kwa sasa Mbwana Samatta anakuwa kaichezea Genk katika Europa League hatua ya Makundi kwa jumla ya dakika 126, mechi ya kwanza alicheza kwa dakika 77, ya pili 15 na 34.

No comments