TFDA NA TBS ZAITAKA KAMPUNI YA BAKHRESA KUONDOA JUISI YA EMBE SOKONI
Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) vimeitaka kampuni ya Bakhresa Group kuondoa sokoni juisi zake za embe ‘Azam Mango Juice’ kwa kuwa na tarehe ya kutengenezwa ambayo haijafikiwa.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa juisi hizo zimekutwa na kasoro katika maboksi yaliyowekea juisi hizo yameandikwa kuwa imetengenezwa Oktoba 19, 2016 wakati siku hiyo bado haijafikiwa na kuwa juisi hizo zitafikia mwisho wa matumizi wak tarehe 19, Oktoba 2017.
Kutokana na tarehe kwenye maboksi hayo kukosewa, inaweza kuleta madhara wakati muda wake wa matumizi utakapokuwa umeisha kama na tarehe ya kuisha muda wake wa matumizi itakuwa imekosewa pia. Tarehe ya kuisha muda wa matumizi hutegemea tarehe ya bidhaa ilipoanza kutumia, hivyo kama tarehe ya kuanza kutumika imekosea, uwezekano wa kukosewa pia kwa tarehe ya kumalizika muda wa matumizi ni mkubwa.
Post a Comment