MWIGULU AAGIZA WALIMU WALIOHUSIKA NA KIPIGO CHA MWANAFUNZI MBEYA WAKAMATWE.
Mkuu wa shule ya Mbeya Day pamoja na baadhi ya walimu wamechukuliwa na jeshi la polis kwa mahojiano zaidi. Tukio hilo lilitokea 28. September.
Jumanne tarehe 24 mwalimu wa vitendo alitoa homework kwa kidato cha 3 A, kwa bahati mbaya mwanafunzi huyo hakuwepo, Jumatano wakati mwalimu anakusanya homework yule mwanafunzi alimwambia mwalimu kuwa jana yake hakuwepo alikuwa anaumwa.
Mwalimu alianza kumpiga makofi darasani lakini akaondoka naye hadi ofisini na kuwaambia walimu wenzake kwamba mwanafunzi huyo hakufanya homework ndiyo walimu wakamchangia kumpiga.
Hali ya mwanafunzi bado siyo nzuri kwani aliumia sana sehemu ya kichwa na machoni. Tayari Waziri Mwigulu Nchemba ameagiza walimu hao kuchukuliwa hatua za kisheria.

Post a Comment