Header Ads

MTATIRO AMKOSOA MAGUFULI.

Tokeo la picha la julius mtatiro

Saa chache baada ya 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuagiza viongozi wote wa Serikali walioalikwa kuhudhuria sherehe za Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa zitakazofanyika tarehe 14 Oktoba, 2016 katika Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu kutohudhuria sherehe hizo na wale ambao walishalipwa fedha ya posho na safari kwa ajili hiyo wazirejeshe. basi jambo uamuzi huo umezua mjadala ambapo Julius Mtatiro Mwenyekiti wa kamati ya uongozi wa chama cha wananchi (CUF) ameandika haya kupitia ukurasa wake wa facebook.

"Confusion.
Mwenge umezunguka na kutafuna mabilioni ukitetewa. Kwenye kuzimwa ndipo watanzania wanafumbwa macho kuwa "serikali yao pendwa" inabana matumizi. Kwa kweli, ni vigumu kujua malengo mwelekeo na dira za uongozi wetu.
Haya twende tu!".


Taarifa iliyotolewa leo tarehe 12 Oktoba, 2016 Ikulu Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Rais Magufuli ametoa maagizo hayo ikiwa ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya awamu ya tano ya kubana matumizi yasiyo ya lazima na kuelekeza rasilimali nyingi katika shughuli za maendeleo ya nchi.

Viongozi waliotajwa kutakiwa kufuta safari zao za kwenda Bariadi ni pamoja na Wakuu wote wa Mikoa, Wakuu wote wa Wilaya, Wakurugenzi wote wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, Mameya na Wenyeviti wote wa Halmashauri za Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya pamoja na watumishi ambao huambatana nao wakiwemo madereva na wasaidizi wao ambao kwa idadi hufikia takribani 1,500.

No comments