Header Ads

MAMLAKA YA HALI YA HEWA NCHINI TMA YATOA TAHADHARI YA MVUA KATIKA MIKOA YA KANDA YA ZIWA.

Image result for MKURUGENZI WA TMA
Mkurugenzi wa TMA ,DK Agness Kijazi.



Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania TMA, imetahadharisha kuhusu uwezekano wa kunyesha mvua kubwa itakayoambatana na ngurumo katika mikoa ya kanda ya ziwa ukiwemo mkoa wa Mwanza.

Taarifa ya utabiri wa mamlaka hiyo inaonesha kuwa mvua hizo zitanyesha kati ya leo na alhamisi wiki hii na kuwaasa wakazi wa mikoa ya Mara, Kagera, Mwanza, Simiyu, Geita, Shinyanga na Kigoma kuchukua tahadhari.

Tayari mvua hizo zimeanza kunyesha katika baadhi ya maeneo jijini Mwanza hali inayoweza kusababisha athari za kimiundombinu hasa barabara kutokana na mitaro mingi ya maji machafu kujaa takataka na kushindwa kupitisha maji.


Kwa upande wa kiwango cha joto, mamlaka hiyo imebainisha kuwa mkoa wa Mwanza kiwango cha juu cha joto kitakuwa sentigredi 26 huku kiwango cha chini kikiwa sentigredi 18.

No comments