Akizungumza Katika Kikao Cha Bodi Ya Barabara Mkoani Hapa Mbunge Wa Geita Mjini Constatine Kanyasu,Amesema Kuwa Kumekuwepo Na Kero Nyingi Kutoka Kwa Wananchi Kutokana Na Kuharibiwa Kwa Miundo Mbinu Tangu Kuanza Kwa Ujenzi Wa Barabara Hiyo Na Kwamba Imechukua Muda Mrefu Hali Ambayo Imepelekea Kuwa Na Wasi Wasi Na Mkandarasi Ambae Anajenga Barabara Na Kwamba Yawezekana Uwezo Wake Kuwa Ni Mdogo.
“Tunamashaka na mkandarasi huyo kwani ni miezi mitatu sasa tangu ujenzi uanze lakini bado hatuoni jitihada zikifanyika katika kumaliza ujenzi huo mimi nafikiria sisi kama bodi tuje twende tukajionee namna ambavyo ujenzi huo unasua sua.”alisema Kanyasu.
Kutokana Na Swala Hilo La Barabara Mwenyekiti Wa Bodi Hiyo Ambae Ni Mkuu Wa Mkoa Wa Geita,Meja Jenerali Mstafu Ezekiel Kyunga Amefafanua Kuwa Ni Wajibu Wa Mkandarasi Kumaliza Ujenzi Huo Katika Wakati Uliopangwa Ili Kupunguza Changamoto Ambayo Wananchi Imekuwa Ikiwakabili Katika eneo Hilo.
Akijibu Hoja Hiyo,Msimamizi Wa Barabara Hiyo Mwandisi Kepucheki Mango,Ameeleza Changamoto Ya Kutokukamilika Kwa Wakati Ujenzi Huo Ni Kutokana Na Kukutana Na Mwamba Kwa Baadhi Ya Maeneo Wakati Wa Ujenzi Huo .
“Ujenzi wa barabara umechelewa kutokana na kukutana na mwamba mgumu wakati wa ujenzi wa barabara hiyo na kwamba kwahiyo uchimbaji umechukua muda mrefu lakini kwasasa mkandarasi ameongeza vifaa vya kazi na anatarajia kuanzia December hataanza kuweka rami”alisema Mango
Post a Comment