Header Ads

WASANII MKOANI GEITA WATAKIWA KUJISAJILI BASATA ILI KAZI ZAO ZITAMBULIWE.



Mwenyekiti wa wasanii mkoa wa Geita (Kushoto) Rose Bonanza akiwa anawasikiliza wasanii waliojitokeza katika kikao hicho kilichofanyika Gambo palace hotel mjini Geita.

Viongozi wa TFDAA chama cha wasanii mkoani Geita wakisikiliza hoja mbalimbali kutoka kwa wasanii.

Baadhi ya wasanii walipokuwa wakichangia juu ya suala la uchangiaji wa damu na changamoto zinazowakabili wasanii mkoani Geita.



Wasanii wakisikiliza kwa makini kutoka kwa viongozi wao.


GEITA.Wasanii mkoani Geita wametakiwa kushikamana na kujisajili katika baraza la sanaa la Taifa BASATA ili kazi zao ziweze kutambulika na kufika mbali zaidi.Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa chama cha wasanii mkoa wa Geita Rose Bonanza wakati akizungumza na wasanii hao katika kikao kilichofanyika katika hotel ya Gambo palace hotel mjini Geita.

Sambamba na hilo wasanii hao wametakiwa kuchangia damu katika hospitali ya mkoa wa Geita kwa lengo la kuokoa uhai wa wagonjwa wakiwemo kina mama na watoto,akizungumzia suala hilo Rose amesema kufanya hivyo ni njia itakayoweza kuwatambulisha wasanii kwa jamii inayowazunguka kwani wao ni kioo cha jamii.

Imeandaliwa na Paul William 

KAMA UNA HABARI AU PICHA WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0765 49  72 39

No comments