Shekhe Yusufu, akiwaeleza waumini namna ambavyo wanatakiwa kuendelea kumcha Mungu na mwisho wa siku ni vyema wakafika katika Nchi ya Saud Arabia kwaajili ya kuhiji.
Waumini wakimsikiliza kwa makini shekhe wakati wa ibada ya shukrani.
GEITA:Mahujaji wanne wakiongozwa na Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Geita,Alhadi Yusufu Kabaju,wamerejea mkoani humo wakitokea nchini Saud Arabia ambako walikwenda kuhiji ikiwa ni moja kati ya nguzo muhimu katika Dini ya Kiislamu.
Akizungumza katika ibada ya kumshukuru Mungu kuwarudisha salama,shehe Alhadi Yusufu Kabaju,amesema kuwa ni jambo la busara sana kumshukuru Mungu kwani amewasaidia katika safari yao kwenda na kurudi salama.
“Ni jambo la kumshukuru mwenyezi Mungu sana na Mtume wake Muhammad (SAW) ni jambo ambalo waislamu tunapaswa kumshuru mwenyezi Mungu sana ,safari ya kiibada ni safari nzito sana kwasababu ukiangalia safari ya kwenda na kurudi ni safari nzito sana huwezi ukaamini kuwa mtu anaweza kwenda safari hiyo na umma wa Dunia nzima mkakutana sehemu moja.”alisema Shehe Kabaju.
Aidha kwa upande wao wahumini wa dini ya kislamu wameshukuru na pia wamefurahia kwa kurudi salama kwa mahujaji ambao walikwenda kuhiji Makkah.
Mahujaji hao wamerejea siku ya Jumamosi wakitokea nchini Saudi Arabia ambako walikwenda kuhiji.
Imeandaliwa na Joel Maduka.
|
Post a Comment