Header Ads

Kupatwa kwa mwezi ni Septemba 16, nchi nzima kushuhudia


BAADA ya tukio la kupatwa kwa jua lililotokea Septemba Mosi, mwaka huu, Mtaalamu kutoka Kitivo cha sayansi, Teknolojia na Elimu ya Mazingira kutoka Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Dk. Noorali Jiwaji, amesema Septemba 16, mwaka huu, itakuwa siku ya kupatwa kwa mwezi.
Kwa mujibu wa mtaalamu huyo, dunia itashuhudia tukio hilo la Septemba 16, mwaka huu la kupatwa kwa mwezi kivuli, ikiwa ni muendelezo wa tukio hilo la kupatwa kwa jua la Septemba Mosi.
Anasema katika tukio la Septemba 16, mwezi utakuwa upande wa pili wa dunia na kwamba nusu ya dunia inatarajiwa kuona tukio hilo la kupatwa kwa mwezi kivuli na kwa hapa nchini litaonekana sehemu zote.
Habari ni kwa mujibu wa magazeti ya Uhuru na Raia mwema

No comments