Header Ads

Waziri Ummy: Kauli ya Rais "Kufyatua watoto" ilikuwa ni utani, Sera ya Taifa ni uzazi wa Mpango



Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema kauli ya Rais kwa Watu Dar kuwa "wafyatuwe" tu watoto maana elimu itakuwa bure ilikuwa ni utani tu kwa Wazaramo,kwa sababu sera ya Taifa mpaka sasa ni uzazi wa mpango.

Kauli hiyo ameitoa leo alipokuwa anaongea na waandishi wa Habari kuweka sawa kauli hiyo ya Rais. Ummy Mwalimu anasema baada ya kauli hiyo kumekuwa na mijadala na kauli za kukinzana na Sera ya Taifa ya Uzazi wa Mpango,Lishe bora na Afya kwa watoto.Mh.Ummy anasema kauli ile isichukuliwe kama ni sera ya Taifa kwa sasa na wala siyo kauli "serious" bali ni utani wa Rais kwa watani zake Wazaramo,na ndio maana Rais alisema "Watani zangu Wazaramo".

Msimamo wa Wizara ya Afya na Serikali kwa ujumla ni sera ya Uzazi wa Mpango ili kuweza kukabliana na ongezeko la Watu Duniani linaloendana na ukuwaji wa uchumi na maendeleo ya watu.Hivyo Watanzania wanahimizwa kuzaa kwa mpango ili kuweza kumudu familia na kuepuka madhara ya uzazi usio na mpango wa "kufyatuwa" watoto.

No comments