Header Ads

MGODI WA DHAHABU WA GEITA WAKUBALI KUTOA MABAKI YA MAWE YA DHAHABU KWA WANANCHI.


Serikali  imesema kuwa mgodi wa dhahabu wa Geita GGM umekubali  kutoa miamba taka(magwangala) kwa ajili ya   wananchi mkoani hapa  hivyo  ni vyema kwa serikali ya mkoa kuhakikisha kuwa inatafuta  eneo kwa  ajili ya shughuli ya uchenjuaji.

Hayo yamesemwa na waziri wa nishati na madini Mh. Prof,Sospeter Muhongo wakati  wa kikao na wachimbaji kilichofanyika katika ukumbi wa mkoa wa Geita,amesema kuwa swala la  magwangala mwisho wake  na majibu yake yatapatikana tarehe 30,ya mwezi wa sita  endapo eneo ambalo      litapatikana litakuwa limekidhi vigezo na sheria  na kuwepo kwa usalama  kwa  eneo hilo.

Aidha  waziri Muhongo ameutaka mgodi wa dhahabu GGM,katika kikao cha  tarehe 30,kuhakikisha kuwa wanaonesha ni kiasi gani cha fedha walizotoa katika maendeleo ya mkoa kwa kipindi cha miaka mitano.

Aidha kwa upande wao wabunge wa majimbo yote ya Geita waliokuwepo katika kikao hicho wametoa maoni yao tofauti juu ya kauli ya kutolewa kwa miamba taka tarehe 30 june.Ambapo Joseph Kasheku Msukuma ambaye ni mbunge wa Geita vijijini amesema kuwa kumekuwa na ahadi hewa kutoka kwa viongozi juu ya mawe hayo kuyatoa kwa wananchi na ameahidi kulifuatilia suala hilo.

No comments