Header Ads

Magari ya Washawasha Yazua Mjadala Bungeni


Magari ya washawasha jana yaliibua mjadala bungeni baada ya mbunge  wa Viti Maalumu, Susan Lyimo (Chadema) kubanwa athibitishe kauli yake aliyoitoa  kuwa serikali ilinunua magari ya Polisi ‘Washawasha” 777 wakati ilitumia 50 pekee wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita.

Mbunge huyo alitakiwa kuthibitisha hilo na Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu kwa kupeleka uthibitisho au kufuta kauli yake baada ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yussuf Massauni kuomba mwongozo kupitia kanuni ya 64(a) na 63(1) akiomba mwongozo wa hatua gani anaweza kuchukuliwa Lyimo.

“Kanuni zipo, zinampa haki kila mbunge na Naibu Waziri ameomba mwongozo kwa kanuni ya 64(a) na 63(1) sasa kwa kuwa Susan hayupo hapa sasa hivi, akirejea jioni mwongozo wangu ni kwamba afute maneno yake au alete uthibitisho,” alisema Mwenyekiti huyo wa Bunge.

Lyimo katika mchango wake kwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, alisema serikali imenunua magari ya ‘Washawasha” 777 mwaka jana wakati wa Uchaguzi Mkuu lakini yaliyotumika ni 50 pekee.

No comments