Header Ads

WACHUNGAJI WAWILI NA MSHIRIKA WAFARIKI KATIKA AJALI YA GARI.

                           Askofu mkuu wa kanisa la FPCT nchini David Batenzi.
Wachungaji wawili wa kanisa la FPCT, na mshirika mmoja wamefariki na wengine wanne kujeruhiwa katika ajali ya gari aneo la Mabama wilayani Uyui walipokuwa wakisafiri kutoka Mishamo wilayani Mpanda mkoani Katavi, wakielekea jijini Mwanza katika mazishi ya mchungaji wao kiongozi.

Akiongea na waandishi wa habari katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete, mchungaji Banyiyezako Selestini (majeruhi), amewataja marehemu kwa majina ya Mchungaji Ndezimana Sefania, na mchungaji Pili Simion, na mshirika ambaye hakufanikiwa kumkumbuka jina mara moja ambaye amefariki akiwa hospitalini.

Aidha akiongea kwa masikitiko askofu wa jimbo la Tabora Mhashamu Issaya Ilumba amewataka madreva kuwa waangalifu wanapokuwa wanawaendesha viongozi mbalimbali na si kanisa hilo bali Taifa zima kuwa waangalifu kuepusha ajali. 


Ajali hiyo imetokea majira ya saa tisa na nusu 21/04/2016, baada ya gurudumu la mbele kushoto, la gari aina ya Toyota Prado lenye namba za usajili TNA kupinduka mara mbili na kusababisha vifo viwili papo hapo na mmoja katika hospitali ya rufaa ya Kitete Tabora.

No comments