MIUNDOMBINU MIBOVU WILAYANI NYANG`WALE MKOANI GEITA NI KIKWAZO KWA KINA MAMA WAJAWAZITO
Ubovu wa miundombinu ya Barabara na ukosefu wa huduma za afya katika kijiji cha Lubando kilichopo kata ya Shabaka wilayani Nyang`wale mkoani hapa,ni sababu ya akina mama wengi hususani wajawazito kujifungulia njiani na wagonjwa kupoteza maisha kutokana na kufata zahanati katika kata ya kasamwa.
Wakizungumza na storm habari,wananchi wa kijiji hicho wamesema kuwa wamekuwa wakitembea umbali wa kilomita 17 na kutokana na ubovu wa barabara ya kuelekea Kasamwa ambapo ndio panapatikana huduma hiyo imekuwa ikipelekea wagonjwa wengi kupoteza maisha na wakina mama kujifungulia njiani.
Bw. John Magagala ni mkazi wa kijiji hicho ameeleza kuwa suala la ubovu wa barabara ni sababu ambayo imekuwa ikipelekea kukosekana kwa usafiri katika kijiji hali ambayo imekuwa ikisababisha wagonjwa wengi kupoteza maisha pindi wanapokuwa njiani kuelekea kutafuta huduma ya kituo cha afya hii ni kutokana na kutokuwapo kwa kituo cha afya kijijini hapo.
Kwa upande mwingine Bi.Naomi Lunemya ni miongoni mwa wahanga amesema kuwa kutokana na kukosekana kwa huduma za afya katika ngazi za vijiji akina mama wengi wamekuwa wakihangaika kutokana na kukosekana kwa huduma ya afya.
Odelo Rastilajula amesema kuwa wanawake wengi wamekuwa wakipata shida kupata huduma ya afya kutokana na umbali wa kilomita 17 kutoka lubando hadi kasamwa hali ambayo imekuwa inasababisha akina mamawengi kujifungulia njiani.
Hata hivyo storm habari ilipomtafuta diwani wa kata ya shabaka kwa njia ya simu kujua anajitihada gani za kuhakikisha anaboresha kata yake ikiwa ni pamoja na miundombinu ambayo wananchi wake wamemlalamikia hakuweza kupatikana.
Post a Comment