Dunia imepata msiba wa mwimbaji wa siku nyingi Prince
Legendary wa muziki Marekani na Duniani Prince Rogers Nelson, mwenye umri wa miaka 57 ambaye aliwahi kuuza takriban albamu milioni 100 na aliwahi kubuni chapa yake binafsi ya muziki uliokuwa na sauti na ala za mchanganyiko wa muziki wa Rock na funk.
Asubuhi ya April 21 2016 Prince amepatikana amefariki dunia katika makazi yake ya huko Minneapolis, taarifa zinasema amekutwa amekwama kwenye lifti katika studio Paisley Park, imeripotiwa kuwa staa huyo inawezekana alikuwa anaumwa kwa kipindi cha muda mrefu ambako kulipelekea hata kulazimika kukatiza Show zake kutokana na kudhohofika kwa afya yake.
Imeripotiwa kwamba wiki iliyopita Staa huyo wa ‘Purple Rain’ alikuwa akirudi nyumbani kutoka kwenye show Antlanta Georgia ambapo alilazimisha ndege yake binafsi kutua kwa dharura Molina na alipelekwa hospitali jirani na gari la wagonjwa ambapo alitibiwa na kuruhusiwa masaa machache baadae.
Prince aliwahi kushinda Tuzo za Grammy saba, nyimbo zake tano ziliongoza chart na zingine 14 ziliingia Top 10 pia alishinda Oscar, best original song ‘Purple Rain’
UNAWEZA KUTAZAMA BAADHI YA KAZI ZAKE HAPA CHINI
- Mwanamuzi maarufu Prince Rogers Nelson, alifariki Alhamisi akiwa na umri wa miaka 57. Alivuma sana kwa nyimbo kama vile I Wanna Be Your Lover.
- Prince alizaliwa Minneapolis, Minnesota na alijifunza kucheza ala nyingi za muziki zikiwemo piano na gitaa.
- Alichomoa albamu yake ya kwanza For You, mwaka 1978, ikifuatiwa na Prince (1979), Dirty Mind (1980) na Controversy (1981).
- Alitoa jumla ya albamu 39, nne akizitoa katika miezi 18 iliyopita.
- Alipatikana akiwa amefariki kwenye lifti. Chanzo cha kifo chake hakijabainika.
- Viongozi mbalimbali na watu mashuhuri wamekuwa wakituma salamu zao za rambirambi, akiwemo Rais Barack Obama.
- Rais Obama amemtaja kuwa mcheza vyombo stadi na mwanamuziki hodari. Mashabiki wamekuwa wakikusanyika nyumbani kwake huko Minneapolis kutoa heshima zao.
- Prince alitambuliwa kuwa mtunzaji bora zaidi wa nyimbo enzi zake akiuza zaidi ya rekodi milioni 100.
- Prince alijishindia tuzo ya Oscar mwaka 1985.
- Prince alishinda tuzo saba za Grammy.
- Alikuwa bado anatoa muziki na kutumbuiza mashabiki. Alitumbuiza kwenye tamasha wiki iliyopita nchini Marekani.
- Inakadiriwa kwamba nyimbo ambazo bado hajazichomoa ambazo ziko nyumbani kwake Paisley Park zinaweza kujaza rekodi 100 za muziki.
Post a Comment