Header Ads

WAKAZI WA NYAKABALE WAMLALAMIKIA MKUU WA WILAYA KUWAITA WAHAMIAJI.


Wakazi wa Kijiji cha Nyakabale kata ya mgusu,wamemlalamikia mkuu wa wilaya ya Geita,Manzie Omary Manguchie kwa kuwaita  wao ni wahamiaji haramu.
Wakizungumza na PAUL BAHEBE katika kijiji hicho wamesema kuwa swala ambalo amelifanya mkuu wa wilaya si jambo zuri  wala la busara kwa kuwaita jina la wahamiaji haramu jambo ambalo limewakela na kuwauma.
Aidha kwa upande wake diwani wa kata ya Mgusu Pastori Ruhusa ,amemwomba mkuu wa wilaya kuacha tabia ya kutoa matamshi yasiyofaa  kwa wananchi wake.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Geita,Manzie Manguchie,amekanusha kuwaita majina hayo.

BONYEZA HAPA CHINI KUSIKILIZA MALALAMIKO YA WANANCHI HAO,DIWANI PAMOJA NA MAJIBU YA MKUU WA WILAYA.

No comments