Header Ads

MSICHANA AFARIKI BAADA YA KULA MCHANGA WA KABURI.

Binti mmoja nchini Kenya amefariki  dunia baada ya kula mchanga wa kaburi
-Mhubiri alimshauri ale mchanga huo kwa madai kuwa ana mizimu.


Familia yake marehemu Alice Nandeje inaomboleza kifo chake. Kifo cha msichana huyo kinahusishwa na dawa aliyonyweshwa na mhubiri mmoja kutoka eneo hilo kwa jina la Tom Onyanja.

Inasemekana baada ya Onyanja kuitwa na kumkagua marehemu, alielezea kuwa ameonyeshwa msichana huyo alikua akisumbuliwa na mizimu ya marehemu baba yake, na hivyo ilikuwa bora amtengenezee dawa.

Inasemekana baada ya kunyweshwa dawa, ndivyo hali ya afya ya msichana huyo ilivyozidi kuwa mbaya hadi akapoteza fahamu.

Hata hivyo mhubiri mwenyewe amejitetea akisema huenda ilitokana na familia ya marehemu kutokuwa na Imani na maombi yake ya uponyaji.

No comments