Header Ads

AJARI MBAYA YA BASI YATOKEA.



Abiria 12 wakiwemo wanaume saba na wanawake watano wamefariki baada ya basi walilopanda la kampuni ya TAKBIR kugongana na lori la mafuta katika kijiji cha Kisonzo wilayani Iramba, Singida.Basi hilo lilikuwa linatokea Dar es Salaam kuelekea mji mdogo wa Katoro ulioko mkoani Geita.
 
Akithibitisha taarifa hizo, Kamanda wa Polisi mkoani Singida, Thobias Sedoyeka amesema ajali hiyo ambayo imesababisha watu 18 kujeruhiwa, imetokea usiku wa kuamkia leo
 
Akielezea mazingira ya ajali hiyo, Kamanda amesema kuwa dereva wa basi, Charles Kaeme alikuwa analipita lori la kampuni ya Cocacola kabla ya kuligonga lori la mafuta. Hata hivyo, dereva wa basi hilo alikimbia baada ya ajali kutokea na Jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta.
 
Naye Mganga Mkuu wa hospitali ya wilaya ya Iramba, Timoth Sumbe amethibitisha vifo hivyo na watu 18 bado wanaendelea kupatiwa matibabu.

No comments