Header Ads

OJADACT: TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA SHERIA YA MAUDHUI YA UTANGAZAJI NCHINI.


Mkutano na waandishi wa habari….19/8/2015  10:30 Asb.. Uchambuzi wa  sheria ya  maudhui  ya  utangazaji kuelekea  uchaguzi  mkuu wa oktoba 25, 2015

Chama  cha  waandishi wa  habari wa kupiga  vita  matumizi  ya  dawa za kulevya  na uhalifu tanzania (ojadact) kinachukua  nafasi  hii  kuongea nanyi waandishi wa habari  juu  ya sheria ya  maudhui  ya  utangazaji ( the  broadcasting  services  content .

Ndugu waandishi wa habari  tunaelewa kuwa, mamlaka  ya  utangazaji  tanzania (tcra) ni  chombo  kilichoundwa  kisheria  na kina wajibu wa kusimamia  sekta  ya utangazaji  nchini  kama jinsi sheria no 12  ya mwaka 2003  iliyounda   chombo  hicho.

Kwa masikitiko makubwa  tunawaambia  ndugu waandishi wa habari  kuwa  sheria ilitangazwa  kwenye  gazeti la serikali  Juni 26, 2015  na kuanza  kutumika . 

Sheria hii imekuwa ni kitanzi kikubwa kwa tasnia ya habari nchini kwani inanyima  uhuru wa vyombo vya habari(M&F) na Haki ya  kupata habari(RTI) wakati wa kuelekea  kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu kama zilivyo sheria za makosa ya kimtandao na takwimu za mwaka 2015 pamoja na miswada ya  sheria ya haki ya kupata taarifa na ule wa huduma za vyombo vya habari ambayo ilizuiliwa kujadiliwa bungeni mwezi Juni, 2015.

OJADACT tumeitazama sheria ya maudhui ya  utangazaji na kuona mapungufu yafuatayo…

·Sheria hii haijahusisha wadau wa habari  na kwa namna  moja  au nyingine  inakosa  Baraka za wadau  jambo linalotia  shaka   na kuwa  kati  ya  sheria  za  zinazotungwa kwa lengo la kukomoa  kundi  fulani la kitaaluma.

·Sheria hiyo ina mkizano mkubwa na misingi  ya kitaaluma ya tasnia ya habari, mfano  kutotambua falsafa ya vyombo vya habari na mlengo wao,kutotaka kutambua kuwa mtu  anaweza kutengeneza habari(Prominence), kudumaza uwezo wa Mwandishi kwenye mahojiano kwa kutofanya majadiliano mafupi ya hitimisho na uchambuzi wa hoja za wahojiwa mwishoni mwa kipindi

· Sheria  hii  ina  imejichanganya  katika utambulisho wa vifungu  vya  kwanza na  maudhui  ya  kifungu  hivyo.(Rejea sehemu ya III kifungu cha 15 ) sehemu  ya  No broadcast on poling day na tazama kifungu cha  maudhui cha 15.

·Sheria imeweka mitego mipana na maana  ya mambo ambayo hayatakiwi,Mfano kifungu cha 15 (2) maneno yafuatayo.. No broadcast any politically – related  matter which may  reasonable upset the balance to be  observed …… Hapo ni wazi kuna mkizano wa maana pana inayoweza kutafsiriwa na mamlaka moja tu yani watunga sheria na sio watumiaji wa sheria.

·Sheria pia imenyakua miongozo ya kitaaluma kwa mwandishi na kuifanya sheria badala   kuiacha katika maadili ya kitaaluma (Media  ethics) ambayo ingeweza kusimamiwa na vyombo husika kama MCT, UTPC, OJADACT, MISA, TAMWANA na vingine. Rejea  msisitizo wa sehemu ya II kifungu cha 4(a) – (i)

RAI:
·Kuwe na maridhiano ya pamoja baina ya TCRA  na wadau wa habari ili kutazama utekelezaji wa  sheria hii  ili  kutominya uhuru wa vyombo vya habari na haki ya kupata taaifa kwa wananchi.

·Serikali iache kuwa na ajenda ya  siri  katika  kuvibana  vyombo  vya  habari  wakati huu  wa kuelekea kwenye  uchaguzi  mkuu badala  yake  ishirikiane  na  vyombo  hivyo  kutengeneza  ajenda  ya  kuwavusha  watanzania salama  kwenye  uchaguzi  huu.

·Wamiliki wa vyombo vya  habari na waandishi wa habari  wawe makini  na sheria  hii

MSIMAMO WA CHAMA

Sheria hii siyo rafiki kwa vyombo vya habari na inalenga kuvibana vyombo hivyo kutofanya kazi iapasavyo kuelekea  uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba, 25 mwaka huu,1-g kama zilivyosheria za makosa  ya  mtandaoni na takwimu  zinazoanza  kutumika  mwezi  Septemba 1, mwaka  huu  ina ile miswada miwili ya haki ya kupata  taarifa  na  huduma  kwa  vyombo  vya  habari.

Imetolewa na;
Edwin Soko
Mwenyekiti 
OJADACT
19.08.2015

No comments