Serikali yawasha moto Bungeni kuhusu madanguro, biashara ya ngono
Serikali
imesema inaandaa mikakati itakayowezesha kudhibiti biashara ya ngono
na uwepo madanguro nchini, hasa kwenye maeneo ya mijini.
Hayo
yamesemwa jana Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile wakati
akijibu swali la Mbunge wa Mtambwe, Khalifa Mohammed Issa aliyehoji juu
mpango serikali katika kudhibiti biashara ya ngono na madanguro ili
kupunguza maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi (VVU) nchini.
Akijibu
swali la Issa, Dkt. Ndugulile alisema Serikali inaandaa mikakati
mbalimbali ikiwemo utoaji wa elimu kuhusu madhara ya biashara ya ngono
kwa jamii pamoja na kuchukua hatua za kisheria kwa wanaojihusisha na
baishara hiyo, pamoja na kudhibiti uwepo wa madanguro.
Katika
hatua nyingine, Dkt. Ndugulile alisema serikali inaendelea kuchukua
hatua katika kudhibiti mila na desturi potofu zinazochangia maambukizi
mapya ya VVU, ikiwemo ukeketaji na urithishaji wa wajane kwa ndugu wa
mume, kwa kutoa elimu kwa jamii juu ya madhara ya mila potofu pamoja na
kutoa hamasa kwa wakunga wa jadi wanaojihusisha na ukeketaji.
Post a Comment