WATUMISHI 3 SINGIDA WAFUKUZWA KAZI KWA UTORO.
Baraza la madiwa la halmashauri ya mkalama mkoani
Singida kwa kauli moja wamewafukuza kazi watumishi watatu wa idara mifugo na
uvuvi,afya na elimu kwa kosa la utoro kazi.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya mkalama
Mheshimiwa James Mkwega amesema hayo kwenye kikao cha Baraza la halmashauri
hiyo,na kuwataja watumishi hao ni Bwana James Kidumo Moses aliyekuwa Afisa
mifugo na uvuvi daraja la tatu,Bi,sera Ogoti Afisa Muuguzi Msaidizi daraja la
pili na Isa Selemani Mtunga fundi sanifu maabara wote hao wamefukuzwa kwa kosa
la utoro kazini.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya
wilaya ya Mkalama Mhandisi Godfrey Sanga amesema halmashauri yake imemteua
Bwana Godluck Mlau kuwa Kaimu Ratibu wa TASAF wilaya ya Mkalama baada ya
aliyekuwepo Bwana Athumani Dule kukutwa na tuhuma za kuongeza kaya zisizo na
sifa ishirini nanane.
Awali akisoma bajeti ya mpango wa makisio ya
maendeleo kwa mwaka wa fedha 2017/2018 Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo
Bwana Loth dia amesema Halmashauri ya Mkalama inatarajia kutumia zaidi ya
shilingi bilioni 18.9.
Post a Comment