Header Ads

WATU WAWILI WANASHIKILIWA NA POLISI MKOANI RUVUMA KWA KUHAMASISHA USHOGA NA USAGAJI.


Jeshi la polisi mkoani Ruvuma linawashikilia watu wawili Bw.Ismail Tindwa na Bw. David Laizer wakazi wa Kinondoni jijini Dar es salaam kwa tuhuma za kuhamasisha ushoga na usagaji vitendo ambavyo ni kinyume na sheria za Tanzania.
Hayo yamesemwa na Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Kamishna Msaidizi wa polisi ACP Zuberi Mwombeji ambapo amesema watuhumiwa hao wamekamatwa kwenye hoteli moja mjini Songea na kwamba tayari wameshatoa uhamasishaji wa ushoga na usagaji kwenye baadhi ya mikoa hapa nchini chini ya mwamvuli wa shirika lisilokuwa la kiserikali la Stay Away Network Activities(sana)ACP.
Kamanda mwombeji amesema watuhumiwa hao wanaofadhiliwa na nchi moja ya ulaya wamekamatwa na madodoso mbalimbali yanayohamasisha ushoga na usagaji.
ACP mwombeji amesema vitendo hivyo ni vya aibu na kinyume na sheria za tanzania hivyo ameitaka jamii kutojaribu vitendo hivyo.

No comments