Header Ads

TANZIA:MWANDISHI WA HABARI WA CHANNEL TEN MKOANI GEITA AFARIKI DUNIA.

Valence Robert (kulia)

Habari tulizozipata hivi punde ni kwamba Mwandishi wa habari wa Channel Ten mkoa wa Geita Valence Robert amefariki dunia leo Jumanne Machi 28,2017 nyumbani kwao kijiji cha Mgana Wilaya ya Misenyi Bukoba mkoani Kagera.



Chanzo cha kifo chake bado hazijajulikana.

Valence Robert pia alikuwa anaandikia gazeti la Tanzania Daima.

Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Geita Daniel Limbe amethibitisha taarifa za kifo cha mwandishi wa habari Valence Robert.

Limbe ameiambia Malunde1 blog kuwa Valence Robert kuwa hivi karibuni aliondoka mkoani Geita akidai anaumwa ingawa baadhi ya watu aliwaambia anakwenda nyumbani kwao kuuguza ndugu yake.

Hata hivyo inaelezwa kuwa Valence Robert alikuwa anaumwa ugonjwa usiojulikana.


Hivi karibuni Valence Robert na Joel Maduka walikamatwa na polisi na kudaiwa kupigwa na polisi wakati aliyekuwa waziri mkuu Edward Lowassa alipofanya ziara mkoani Geita.

 Kupitia ukurasa wake wa Facebook,mkurugenzi wa Malunde1 blog,Kadama Malunde...ameandika

“Nilifahamiana naye mwaka 2011 nikiwa Mhariri Mkuu wa Habari Radio Faraja Fm Stereo,alikuwa ananitumia habari nyingi za mkoa wa Geita.Hata Nilipotoka Radio Faraja mwaka 2012 Kijana Valence Robert aliendelea kuwa rafiki yangu,alinipigia simu mara kadhaa,usiku na mchana…aliniambia “Kaka kuna stori nimekutumia kwenye email yako…icheki kisha itupie kwenye blog yetu ya Malunde1 blog”….wakati mwingine aliniambia “Kaka niko mbali na mtandao,kaa vizuri nikusimulie utaandika mwenyewe huku kuna tukio”,…..Aliniambia anaandikia Gazeti na Tanzania Daima na hata alipoanza kuripoti Channel Ten aliambia ...

Hakuogopa hatari mbele ya habari aliyoitaka...Valence Hakusita kunitafuta kila alipofika Shinyanga mjini….Daah!! Kweli duniani tunapita tu tangulia mshikaji wangu Valence Robert…

Poleni sana kwa msiba  familia ya Valence Robert,waandishi wa habari mkoa wa Geita na nchi kwa ujumla.

Daima ntakukumbuka jama yangu..R.I.P Kaka!!”

No comments