Header Ads

WANANCHI WAGOMA KUTIBIWA KWA SIKU 2 KUSHINIKIZA MGANGA WA ZAHANATI YA KIJIJI KUONDOLEWA.


Wananchi wa kijiji cha Nyakilenda kata ya Itaba wilayani Kibondo mkoani Kigoma, wamemkataa mganga wa zahanati ya kijiji jirani cha Mkabuye wanakopata huduma za afya na kugoma kutibiwa kwa siku mbili mfululizo wakishinikiza kuondolewa kwa mganga huyo kutokana na tabia za kuwanyanyasa wagonjwa na kukataa kuwatibu wanapofika katika zahanati hiyo.
Wakizungumzia hali ya utoaji huduma katika zahanati hiyo wamesema mganga huyo aliyejulikana kwa jina la edward banguze amekuwa akifanya vitendo visivyo vya kimaadili na wameamua kuchukua hatua hiyo kutokana na kunyanyaswa kwa muda mrefu hali ambayo imekuwa ikiwalazimisha kusafiri umbali mrefu kwenda vijiji vingine kupata huduma.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya kibondo juma mnwele amewataka wananchi hao kuendelea kupata matibabu katika zahanati hiyo katika kipindi hiki ambacho halmashauri inatafuta ufumbuzi wa kudumu wa tatizo hilo baada ya kumuhamisha mtumishi huyo.

No comments