TARIME KUANZA KILIMO CHA MASHAMBA MAKUBWA YA MIWA.
Serikali
wilayani Tarime mkoani Mara,imetangaza kuanza kulima mashamba makubwa ya zao la
miwa,ikiwa ni pamoja na ujenzi wa kiwanda kikubwa cha kuchakata zao hilo,ili
kuwezesha uzalishaji wa sukari kama moja ya mkakati wa wilaya wa kuwapatia
wananchi wa wilaya hiyo zao mbadala na hivyo kuachana na kilimo cha zao haramu
la bangi.
Akitangaza
mpango huo ambao utawezesha watu elfu hamsini kupata ajira,mkuu wa wilaya ya
Tarime Bw Glorious Luoga,amesema tayari mpango wa uwekezaji wa kilimo hicho
umekamilika,huku uongozi wa wilaya ukitenga ardhi yenye ukubwa wa zaidi ya
ekari 150,000, kwa ajili ya kilimo cha zao hilo la biashara.
Kwa
sababu hiyo mkuu huyo wa wilaya ya Tarime,amesema kuwa kuanzishwa kwa kilimo
hicho cha miwa katika eneo la Tarime,ni moja ya mkakati wa wilaya katika
kupambana na kilimo cha zao haramu la bangi.
Hata
hivyo kiongozi huyo wa serikali wilayani Tarime,amesema katika kuinua hali za
wananchi wa wilaya ya Tarime kiuchumi,uongozi wa wilaya umekubaliana na kampuni
ya uchimbaji wa madini ya Acacia,kuanzisha mashamba makubwa ya ushirika kupitia
kilimo hicho zao hilo la miwa.
Post a Comment