Mkuu wa Mkoani wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga ,amewaagiza wakuu wa wilaya wote kuhakikisha wanasimamia vyakula vilivyopo ikiwan ni pamoja na kudhibiti uuzwaji wa nafaka kwenye wilaya na mikoa jirani.
Mh,Kyunga ametoa maagizo hayo wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea maghala ya vyakula kwenye wilaya za Geita,Bukombe na Mbogwe lengo likiwa ni kujionea hali ya chakula Mkoani hapa.
Amesema kuwa ni vyema kwa wakuu wa wilaya kudhibiti chakula kilichopo ikiwa ni pamoja na kuwaelekeza wananchi kutunza mazao katika kipindi hiki ambacho mvua zimekuwa ni za kusuasua
“Niwaombe wakuu wa wilaya zote kuwa waangalifu na kukilinda chakula kilichopo ili Wilaya na Mikoa ya jirani isije ikachukua na kutuacha hatuna tena chakula lazima hiki kilichopo kitunzwe na kuhifadhiwa na muwahimize wananchi walime mazao ambayo yanakubaliana na mvua kidogo Mfano,Viazi Mtama na muhogo”Alisema Kyunga
Akisoma taarifa ya mazao na hali ilivyo kwasasa kwenye soko la kibiashara Katibu wa wafanya Biashara Soko la ccm Kata ya Katoro,Charles Mlale alisema kuwa Bei ya nafaka kwa mwaka huu imepanda zaidi ikilinganishwa na mwaka jana kwani mwaka jana gunia la mahindi walikuwa wanachukulia kiasi cha sh elfu themanini kwa sasa imefika kiasi cha laki na ishirini
Akizungumza kwa niaba ya wakuu wa wilaya ,Mkuu wa wilaya ya Bukombe Josephat Maganga amemhakikishia Mkuu wa Mkoa kufanyia kazi maagizo aliyoyatoa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha hakuna mtu ambaye atatoka mikoa ya jirani au wilaya kuja kununua mazao yaliyopo kwenye wilaya wanazozisimamia .
Post a Comment