Tangazo la kuacha ungariba lamponza, atozwa faini ya ng’ombe watatu
Serengeti. Uamuzi wa kutangaza kuacha ungariba umeponza ajuza Goshiyi Maduhu (72), mkazi wa kijiji cha Wagete Kata ya Rigicha Wilaya ya Serengeti mkoani Mara baada ya ukoo kumpiga faini ya ng’ombe watatu kwa kosa la kuacha mila.
Pamoja na ungariba, Maduhu pia alikuwa mganga wa kienyeji aliyekuwa akifanya matambiko pale jamii inapokumbwa na majanga.
Akizungumza na Mwananchi nyumbani kwake Maduhu amesema aliamua kuacha ungariba na uganga baada ya kuokoka, uamuzi uliowachukiza wana ukoo na kuazimia kuchukua ng’ombe wake watatu, ambao walichinjwa na kuliwa kama adhabu.
Hata hivyo, Ofisa Mtendaji wa Kata ya Rigicha, Musami Chimaja amesema tayari ofisi yake kwa kushirikiana na jeshi la polisi imewatia mbaroni watu watatu wanaodaiwa kuhusika na uchukuaji wa ng’ombe nyumbani kwa ajuza huyo kinyume cha sheria.
Post a Comment