Header Ads

CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI CHALAANI SHAMBULIO LA WAANDISHI MKOANI GEITA

Mwenyekiti wa chama cha waanishi wa habari(GPC)Mkoani Geita  Daniel Limbe akitoa tamko na kulaani vikali juu ya tukio walilofanyiwa waandishi wa habari.
Waandishi wa habari wakimfatilia kwa makini mwenyekiti wa GPC

Viongozi wa GPC wakiwa kwenye kikao cha waandishi wa habari kulia ni Victor Bariety ambaye ni makamu mwenyekiti wa chama hicho na kushoto ni katibu wa GPC Salum Maige .


Chama cha waandishi  wa habari Mkoani  Geita(GPC) kimelaani vikali kitendo cha  kushambuliwa kwa waandishi habari   na jeshi la polisi wakati   wakiwa katika majukumu yao ya kikazi.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema jana ,mwenyekiti wa chama hicho Mkoani humo,Daniel Limbe,amesema kuwa swala lililofanyika kwa kushambuliwa kwa waandishi wa habari ni mwendelezo wa jeshi  hilo kuminya uhuru wa habari kwa watanzania ambao walipenda kujua ni kipi ambacho kilijili siku ya juzi.

“Kama chama cha waandishi Mkoani Geita,tumesikitishwa sana na kitendo cha jeshi polisi kuwavamia waandishi na kuwapiga sisi kama chama tumeona hatuwezi kukaa kimya swala hili tunalilaani vikali kwani ni mwendelezo wa uonevu kwa waandishi wa habari hapa nchini kupitia kwa jeshi la polisi”Alisema Limbe

Hata hivyo Limbe amemtaka Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi,Mwigulu Nchemba  kujitokeza hadharani na kutoa tamko juu ya tukio lililofanywa na askari ambao wamehusika na kitendo cha kuwapiga waandishi wa habari .

“Sisi kama chama cha waandishi wa habari mkoa wa Geita  tunamwomba sasa Waziri wa Mambo ya ndani , Mh Mwigulu Nchemba  kujitokeza hadharani na kutoa tamko dhidi ya jeshi la Polisi kutokana na unyanyasaji wanaofanya kwa wanahabari na vyombo vya habari kimsingi tunaomba asimame na kuwaeleza  Watanzania kuhusiana na tukio la jana kama  vitendo  vilivyo fanywa na jeshi la Polisi kama ni maagizo yake au  maagizo ya mkuu wa polisi  wa mkoani Geita  ama ni ukiukwaji wa taratibu za kiutumishi wa vijana wa jeshi la polisi”Alisisitiza Limbe

Aidha baadhi ya wananchi Mkoani humo wamelaani kitendo walichofanyiwa waandishi wa habari kuwa swala hilo ni ukiukwaji wa sheria za nchi na kutokutoa uhuru vyombo vya habari kuripoti vitu ambavyo vinakuwa vimejitokeza.

Hali hiyo  imekuja ikiwa ni siku moja tangu kutokea kwa tukio hilo wakati waandishi  wa habari wa storm fm na channel ten  walipokuwa wakifatilia taarifa ya kukamatwa kwa waziri mkuu mstaafu wa awamu ya nne na mjumbe wa kamati kuu wa  Taifa chadema,Edward Lowassa kukamatwa akiwa anatokea Mkoani Kagera wakati alipokuwa akisalimiana na wananchi kwenye eneo la stend ya zamani.

No comments