Warioba: Maadili yameporomoka kwa viongozi na jamii
Jaji Mstaafu, Joseph Sinde Warioba amevishauri vyombo vinavyo simamia maadili kubadilika kiutendaji na kuachana na masuala ya kisiasa na amependekeza kuwa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU), na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali kupewa nguvu ili zifanye kazi zake kiurahisi.
Aliyasema hayo Jijini Dar es salaam alipokuwa akichangia kwenye mdahalo wa wadau ulioandaliwa na TAKUKURU kuhusu kujenga na kukuza maadili, haki za binadamu, uwajibikaji, utawala bora na mapambano dhidi ya rushwa.
Warioba alisema ni jambo lisilofichika kuporomoka kwa maadili si kwa jamii pekee, bali hata kwa baadhi ya viongozi.
“Lazima kuwe na misingi ya uongozi,maadili yameporomoka sana na ni ngumu kuyarudisha”alisema Warioba.
Aidha, Warioba alisema maadili hayajengwi na sheria wala hayasimamiwi na taasisi bali yanajengwa na kusimamiwa na jamii.
Post a Comment