Header Ads

Ajali ya Magari 3 Yaua 11 Dakawa, Moro

BREAKINGNEWSHabari zilizotufikia hivi punde ni kuhusu ajali mbaya iliyotokea eneo la Veta Dakawa mkoani Morogoro ikihusisha basi la Kampuni ya Otta Classic lenye namba za usajili T 201 DGK likitokea Bukoba kuelekea Dar es Salaam lililogongana na lori la mafuta lililokuwa limepaki pembezoni mwa barabara.
Taarifa ya awali kuhusu tukio hilo zinasema watu 11 wamefariki dunia wakiwemo madereva wote wawili na na wasaidizi wao huku wengine ambao idadi yao bado haijajulikana wamejeruhiwa.
Miili ya baadhi ya marehemu imepelekwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa utambuzi na baadhi ya majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu kwenye hospitali ya St. Joseph inayomilikiwa na Kanisa Katoliki.
Zifuatazo ni taswira kutoka eneo la ajali;
432165

No comments