Header Ads

VIDEO: Polepole amejibu tena kuhusu msimamo wake wa serikali 3

Hivi karubuni katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole, kukubali madaraka ya usemaji wa chama hicho, alisikika aking’ang’ania msimamo wake wa Muungano wa Serikali Tatu, unaopingana na matakwa ya chama hicho.
Polepole alitoa msimamo huo akiwa kwenye ofisi ndogo za makao makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari mbele ya mtangulizi wake, Nape Nnauye aliyeonekana kutoridhishwa sana na majibu hayo.

Leo Desemba 22, 2016 kupitia kipindi cha Clouds360 kinachorushwa na televisheni ya Clouds Polepole ameulizwa swali hilo na mtazamaji ambapo alitumia zaidi ya dakika 8 kujibu swali hilo kama anavyoonekana kenye video hapo chini...

No comments