Header Ads

Ripoti ya google juu ya nini Watanzania wamekitafuta sana kwenye mtandao

Kampuni ya Google imetoa ripoti ya mambo ambayo Watanzania walitafuta sana mtandaoni mwaka 2016.

Maelezo waliyotafuta yameangazia masuala ya afya, biashara na fedha na pia burudani.
Pia, yapo masuala ya kijamii.

Walichotafuta sana mtandaoni ni matokeo ya darasa la saba 2016, zikifuatwa na Beka Boy, mtandao wa burudani.

Walitafuta pia Mkekabet, ambao ni mtandao wa kuweka dau kuhusu matokeo ya mechi za kandanda na mashindano mengine ya kimichezo.

Walitafuta pia habari kuhusu matokeo ya kidato cha nne 2016, pamoja na Raymond, ambapo walitaka habari na maelezo kumhusu mwanamuziki Hekima Raymond mzaliwa wa Moshi, Tanzania.

Walitaka kujua kufanya nini?

Watanzania walitaka sana kujua jinsi ya kuweka tone la dawa jichoni, ikifuatwa na jinsi ya kuwapata wawekezaji na wafadhili.

Walitaka pia kujua sana jinsi ya kukuza nyusi na pia jinsi ya kujua mwanamke atajifungua tarehe gani.

Huenda kukoroma likawa tatizo linalowasumbua wengi kwani, kwenye nambari tano, Watanzania walitaka kujua jinsi ya kuacha kukoroma.

Kujua maana

Katika maneno ambayo Watanzania walitafuta sana maana, nambari tatu kuna neno la kushangaza 'Bae'.

Ni ufupisho wa neno 'Babe', mtoto au mpenzi kwa Kiingereza. Pia ni akronimi ya before anyone else, kabla ya wengine wote.

Kuna wimbo wa Sauti Sol na Alikiba kwa jina Unconditionally Bae, ambao huenda uliwafanya wengi kutaka kujua maana ya 'Bae'.

Wakenya hutaka kujua nini mtandao
ni?
Mambo yaliyotafutwa sana Tanzania 2016:

matokeo ya darasa la saba 2016

beka boy

mkekabet

salehe jembe juni 26 2016

Malazi Arusha

euro 2016

matokeo ya kidato cha nne 2016

yinga media

muungwana

Raymond

Walichotaka kujua sana kufanya:

Jinsi ya kuweka tone la dawa jichoni

Jinsi ya kupata wawekezaji/wafadhili

Jinsi ya kukuza nyusi

Jinsi ya kujua tarehe ya kujifungua

Jinsi ya kuacha kukoroma

Jinsi ya kufanya cd kuweza kuifungulia kompyuta

Jinsi ya kuomba na ubani

Jinsi ya kupika danish na croissant

Jinsi ya kuanzisha kiwanda cha chokoleti

Jinsi ya kujua iwapo mtoto amegeuka

Ni nini:

Malengo ni nini

Bae maana yake ni nini

Elimu rasmi ni nini

Ndoa ya wake wengi ni nini

Hesabu ya jumla ni nini

Matumizi ya pesa ni nini

Soko la kubadilishana sarafu za kigeni ni nini

Mfumo ni nini

Ghala ni nini

No comments