Header Ads

Wisconsin: Trump amtaka Clinton kukubali kushindwa

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amemshutumu Hillary Clinton kwa kuunga mkono kuhesabiwa upya kwa kura katika jimbo la Wisconsin.
Bw Trump amemkumbusha mpinzani wake wa Democrat kwamba alikiri kushindwa katika matokeo ya uchaguzi uliopita.
Shughuli ya kuhesabu kura upya katika jimbo hilo ilianzishwa na mgombea wa urais kupitia chama cha Green Party Jill Stein.
Trump aliibuka mshindi kwa uchache wa kura katika Jimbo hilo.
Stein pia anapigania kuhesabiwa kura upya katika jimbo la Michigan na Pennsylvania akidai kuwa kulikuwa na makosa katika shughuli ya kuhesabu kura.
Mgombea huyo anataka kuhakikisha kuwa wahalifu wa mtandaoni hawakumsaidia bw Trump kushinda.
Wasiwasi kwamba huenda Urusi iliingilia uchaguzi huo umetolewa siku kadha kabla ya shughuli hiyo.

No comments