Wakazi wa wilaya ya Ukerewe, wanalazimika kula mlo mmoja kutokana na upungufu wa chakula, uliosababishwa na hali ya ukame.
![]() |
Baadhi
ya wakazi wa wilaya ya Ukerewe, wanalazimika kula mlo mmoja kwa siku kutokana
na kukabiliwa na upungufu wa chakula, uliosababishwa na hali ya ukame pamoja na
zao la muhogo ambalo ni tegemeo kubwa la chakula kwa wananchi wa wilaya hiyo
kuugua ugonjwa wa Batobato kali.Hali hiyo imebainishwa na mwenyekiti wa halmashauri
ya wilaya ya Ukerewe Gorge Nyamaha.
Diwani
wa kata ya Bukanda Willibart Mbando ameiomba ofisi ya mkuu wa wilaya ya Ukerewe
kupitia kamati ya maafa kutoa vibali kwa wafanyabiashara vya kuagiza chakula
cha msaada pamoja na cha bei nafuu ili kusaidia kupunguza makali ya njaa, huku
diwani wa kata ya Muriti Makole Chilato akisema upungufu huo wa chakula katika
baadhi ya kaya umechangia kushuka kwa mahudhurio ya wanafunzi mashuleni.
Samson
Ibrahim ni mkuu wa idara ya kilimo, umwagiliaji na ushirika wilayani Ukerewe
anasema kulingana na hali ya mavuno msimu uliopita, ilitarajiwa kuwa wilaya
hiyo ingekuwa na ziada ya tani 2,735 hadi kufikia mwezi Aprili mwakani badala
yake hali ya ukame wa muda mrefu imesababisha chakula hicho kutofikia muda huo.

Post a Comment