PICHA:TRUMP NA OBAMA WALIPOKUTANA IKULU YA WHITE HOUSE.
Wanasalimiana lakini macho yako wapi.... taama mdomo wa Trump
Bw Trump kwenye kampeni alimweleza Bw Obama kama rais mbaya zaidi kuwahi kuongoza Marekani.
Rais Obama naye alisema Mwanarepublican huyo hana sifa na uwezo wa kuwa kiongozi wa Marekani.
Mfanyabiashara huyo tajiri kutoka New York, ambaye sasa ni rais mteule, kwa muda mrefu alitilia shaka uhalali wa habari kwamba Obama alizaliwa Hawaii, na alikejeliwa hadharani na Rais Obama.
Wawili hao walishauriana kwa zaidi ya saa moja afisi ya rais katika ikulu ya White House mnamo Alhamisi na walipojitokeza kwa wanahabari, walijaribu kuficha uadui kati yao.
Waliongea maneno mazuri kuhusu umoja na umuhimu wa kupokezana madaraka kwa amani.
Lakini picha zilizopigwa zinaonesha jambo tofauti, ukiangalia sura na mikono...
Nikiangalia sana pale mbali, haya masaibu yote yatapita...
Tena, sasa Obama anamwangalia Trump.... lakini Trump anaamua, la hasha, SIWEZI kumwangalia machoni
Fikira za Trump zinaonekana kuyumba ... labda kwa kukumbuka aibu iliyotokana na utani kuhusu kuzaliwa kwa Obama mwaka 2011.
Kupeana mikono kwisha sasa, na ni furaha sana kwa Trump .... lakini anaonekana kutoyaamini anayoyasema Rais Obama
Wawili hao walicheka wakati mmoja walipotaniana.
Melania Trump na Michelle Obama wakiwa ikulu ya White House







Post a Comment