Header Ads

Pande mbili zinazovutana ndani ya CUF zafikishana mahakamani.


Upande mmoja wa uongozi wa chama cha wananchi CUF unaopinga maamuzi ya ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini kwa kumtambua Prof Ibrahimu Lipumba kama mwenyekiti wa chama hicho, umeamua kufungua shauri mahakama kuu kuitaka mahakama kutoa zuio la msajili wa vyama kuacha kufanya kazi za kisiasa.
Shauri hilo limefunguliwa katika wakati ambao vigogo wawili wa ngazi ya juu wa chama cha CUF Prof Lipumba na Maalim Seif wakionekana dhahili kukigawa chama hicho, ambapo upande unaomuunga mkono Maalim Seif unasema umeamua kufungua kesi kwa lengo la kuiomba mahakama kuu kutoa zuio kwa msajili wa vyama vya siasa kuachana na shughuli hiyo kwa madai amekuwa chachu ya mvutano ndani ya chama hicho.
Wakati kila upande wa vigogo hao wawili wakionekana kuwa na uchu wa kushinda katika mvutano huo wa uongozi, jumuiya ya vijana wa CUF mkoa wa Dar es Salaam wao wanaamini chini ya uenyekiti wa Prof Ibrahimu Lipumba chama chao kitakuwa salama zaidi.
Licha ya viongozi wa juu wa chama hicho kugawanyika vipande, taasisi nyingine ambazo zimekumbwa na mgawanyiko huo ni pamoja na jumuiya ya vijana, bodi ya udhamini ya chama hicho, ikiwa ni pamoja na wanachama wenyewe wa CUF.

No comments