Header Ads

Mkoa wa shinyanga watajwa kuwa kinara kwa ndoa na mimba za utotoni.

 Mkoa wa shinyanga unatajwa kuwa kinara kwa ndoa na mimba za utotoni ambapo asilimia 59 ya watoto wa kike huolewa chini ya umri wa miaka 18 wengi wao ikiwa kutoka familia maskini na maeneo ya vijijini.
Wakati dunia ikijiandaa kuadhiisha siku ya mtoto wa kike duniani ambayo huadhimishwa kila oktoba11,wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto inasema katika tafiti ambayo imefanywa na ofisi ya taifa ya takwimu imeonyesha mkoa wa shinyanga unaongoza kwa kuwa na tatizo hilo ikifuatiwa na mikoa ya Tabora na Mara ambapo serikali inasema haitosita kuwachukulia hatua wazazi ambao huwaozesha watoto wao chini ya umri wa miaka 18.
Wadau mbalimbali waliojikita katika kulinda haki za mtoto wa kike wanasema ni vyema elimu ikaendelea kutolewa kwa watoto wa kike tangu ngazi ya elimu ya awali ili watambue haki zao mapema kutokana na athari za ndoa za utotoni ikiwemo athari za kihisia na kisaikolojia.

Maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani kitaifa yanatarajiwa kufanyika mkoani Shinyanga yakishirikisha wizara na taasisi mbalimbali za serikali na binafsi huku kauli mbiu ikiwa mimba na ndoa za utotoni zinaepukika,chukua Hatua kumlinda mtoto wa kike

No comments