Header Ads

RAIS MAGUFULI ATIMIZA AHADI YAKE KWA MREMA.

RAIS John Magufuli, amemkumbuka Mwenyekiti wa TLP, Augustino Mrema kwa kumteua kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, kwa kipindi cha miaka mitatu, kuanzia jana.
Taarifa iliyotumwa jana kwa vyombo vya habari na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, Ikulu, Gerson Msigwa, imeonesha uteuzi huo wa Mrema, umefanyika sambamba na uteuzi wa viongozi na watendaji wa taasisi mbalimbali za serikali.
Mbali na uteuzi huo, Rais Magufuli katika taarifa hiyo, pia amepandisha vyeo maofisa 25 wa Jeshi la Polisi Tanzania kutoka cheo cha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) na kuwa Naibu Kamishna wa Polisi (DCP).
Aidha amepandisha cheo maofisa wengine 34 wa jeshi hilo, kutoka cheo cha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) na kuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP).
Uteuzi Augustino Lyatonga Mrema.
Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole kwa kipindi cha miaka mitatu, kuanzia leo tarehe 16 Julai, 2016.
Augustino Lyatonga Mrema anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji Mstaafu Eusebia Nicholaus Munuo ambaye muda wake umemalizika.
Prof. William R. Mahalu ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Uteuzi huu umeanza jana Julai 16, 2016.
Prof. Mohamed Janabi ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Uteuzi huo umeanza tarehe Julai 15, 2016.
Prof. Angelo Mtitu Mapunda ameteuliwa kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kwa kipindi cha miaka mitatu.
Uteuzi huo umeanza Julai 15, 2016.
Sengiro Mulebya ameteuliwa kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kwa kipindi cha miaka mitatu.
Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016. Oliva Joseph Mhaiki ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC). Uteuzi huo umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
Mwl. Winifrida Gaspar Rutaindurwa ameteuliwa kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC).
Uteuzi huo umeanza Julai 15, 2016. Dk Charles Rukiko Majinge ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili. Uteuzi huo umeanza leo Julai 16, 2016.
Dk Julius David Mwaiselage ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road. Uteuzi huo umeanza Julai 15, 2016.
Kupandishwa vyeo SACP kuwa DCP. Essaka Ndege Mugasa Adamson Afwilile Mponi Charles Ndalahwa Julius Kenyela Richard Malika Revocatus Geofrey Yesaya Kamwela Lucas John Mkondya John Mondoka Gudaba Matanga Renatus Mbushi Frasser Rweyemamu Kashai Ferdinand Elias Mtui Germanus Yotham Muhume Fulgence Clemence Ngonyani Modestus Gasper Lyimo Mboje John Shadrack Kanga Gabriel G.A. Njau Ahmed Zahor Msangi Anthony Jonas Rutashubulugukwa Dhahir Athuman Kidavashari Ndalo Nicholus Shihango Shaaban Mrai Hiki Simon Thomas Chillery Leonard Lwabuzara Paul Ahmada Abdalla Khamis Aziz Juma Mohamed Juma Yussuf Ally Kupandishwa vyeo ACP kuwa SACP. Fortunatus Media Musilimu Goyayi Mabula Goyayi Gabriel Joseph Mukungu Ally Omary Ally Edward Selestine Bukombe Sifael Anase Mkonyi Naftari J. Mantamba Onesmo Manase Lyanga Paul Tresphory Kasabago Dadid Mshahara Hiza Robert Mayala Lazaro Benedict Mambosasa Camilius M. Wambura Mihayo Kagoro Msikhela Ramadhani Athumani Mungi Henry Mwaibambe Sikoki Renata Michael Mzinga Suzan Salome Kaganda Neema M. Mwanga Mponjoli Lotson Benedict Michael Wakulyamba Wilbroad William Mtafungwa Gemini Sebastian Mushi Peter Charles Kakamba Ramadhan Ng’anzi Hassan Christopher Cyprian Fuime Charles Philip Ulaya Gilles Bilabaye Muroto Mwamini Marco Lwantale Allute Yusufu Makita Kheriyangu Mgeni Khamis Nassor Ali Mohammed Salehe Mohamed Salehe Mohamed Sheikhan Mohamed

No comments