Kikwete Akubali Ombi La Mheshimiwa Rais Fikipe Nyusi Wa Msumbiji Kushiriki Mazungumzo Ya Amani Nchini Humo
Mheshimiwa Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amepokea ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Msumbiji Mheshimiwa Filipe Nyusi.
Ujumbe huo uliwasilishwa jana jijini Dar es Salaam na Mjumbe Maalum wa Rais Nyusi Meja Jenerali Mstaafu Mariano de Araujo Matsinhe ambaye aliongozana na Mshauri wa Diplomasia wa Rais Nyusi Kanali Manuel Mazuze, Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania Mheshimiwa Monica Patricip Clemente Mussa na Afisa wa Ubalozi wa Msumbiji nchini Rachide Usualle.
Mheshimiwa Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipata picha ya kumbukumbu na ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Msumbiji Mheshimiwa Filipe Nyusi
Post a Comment