Header Ads

Ulinzi shirikishi walaumiwa kujihusisha na uhalifu Kahama

Ulinzi shirikishi sungu sungu umeingia dosari katika mtaa wa Inyanga kata ya mhungula wilayani Kahama mkoani shinyanga kwa wananchi kupigwa na kunyang'anywa mali zao.

Wakizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katani hapo wananchi hao wamesema sungu sungu wamekuwa na tabia ya kuwanyang'anya mali zao kwa kile walichokiita ni wizi hivyo wanaiomba serikali ya mtaa huo kuwachunguza kabla hali haijawa mbaya zaidi wakisisitiza wataamua kujichukulia Sheria kupambana na sungu sungu hao.

Kwa upande wake mwenyekiti wa huo nestory Shija amewataka wananchi hao kutoa taarifa pindi wanapofanyiwa vitendo hivyo kwani uongozi haujaruhusu vitendo hivyo.

Ameongeza kuwa mtu anaekamatwa na sungu sungu ahakikishe ana hoji kiongozi wa kikosi hicho wa usiku huo kwani kuna orodha ya watu wanaohusika kulinda pamoja na mkuu wa kikosi hicho.

"Kikosi chetu kiko makini kimekuwa kikimkata mtu awe boda boda hawapigwi wala kunyanyaswa kwa chochote wanalazimika kukesha nao walinzi wetu."

"hilo tutalifanyia kazi wanajiamulia kuwa walinzi wa mtaa kwa ajili ya kuwapora wananchi".

Wakati huo huo wananchi wa kata hiyo ya mhungula wameamua kuanzisha mradi wa gulio kwa ajili ya Maendeleo ya kata hiyo.

Akizungumza katika mkutano huo wa hadhara mhasibu wa kamati ya gulio Bi.Doris amesema kuwa lengo la kuanzisha soko hilo ni kwasaidia wakazi wa kata na Maendeleo ya kata.

Gulio hilo linataraji kufunguliwa rasmi tarehe 30 June mwaka huu huku wananchi wakionesha wasi wasi wao juu ya ulinzi na usalama pindi litakapofunguliwa.

Nae mwenyekiti wa mtaa wa Inyanga kwa niaba ya Diwani wa kata hiyo Bwana Ignas shaban amewahakikishia wananchi hao kuwa kutakuwa na ulinzi na usalama wa kutosha litakapofunguliwa.

No comments