Trump Asisitiza Waislamu Wasiingie Marekani
MGOMBEA wa kiti cha urais wa kupitia chama cha Republican nchini Marekani, Donald Trump, amesisitiza kuwa, mauaji ya watu 50 yaliyotokea kwenye Klabu ya wapenzi wa jinsia moja, yamethibitisha msimamo wake wa kutaka waislamu wapigwe marufuku kuingia humo.
Katika hotuba yake kwenye jimbo la New Hampshire, Trump amesema mfumo wa Idara ya uhamiaji nchini Marekani, umeruhusu familia ya Omar Marteen, aliyetekeleza mauaji hayo kuingia nchini Marekani.
Alidai kuwa, bado mfumo huo umeendelea kuruhusu wauaji wengine kuingia nchini humo bila vikwazo.
Alisema, sababu moja wapo inayochochea muuaji kuwepo nchini Marekani, ni familia ya Marteen kuingia nchini humo.
Aliongeza kuwa, mfumo wa idara ya uhamiaji isiyotekeleza wajibu wake, bado hairuhusu kujua ni nani anayepaswa kuingia Marekani ili raia wa nchi hiyo walindwe.
Kwa upande wa Mgombea urais kupitia Democratic, Hillary Clinton, akitoa risala za pole kwa waathiriwa wa mkasa huo, alisema Trump ni kama mtoto anayesema ovyo kwa namna anavyougeuza mkasa huo wa kitaifa kujipongeza binafsi.
Akizungumza jimboni Ohio, Hillary, amekosoa mpango wa mpinzani wake ambaye ni Trump, kuwazuia waislamu kuingia Marekani
“Hatua hiyo ya uchochezi ya vitisho kuzuia familia na marafi ki wa kiislamu kuingia marekani, pia mamilioni ya wafanyabiashara na watalii waislamu kuingia nchini, inaumiza sehemu kubwa ya waislamu wanaopenda uhuru na kuchukia ugaidi,” alisisitiza.
Naye Rais wa Marekani, Barack Obama alisema, hakuna ushahidi kuwa aliyetekeleza mashambulizi hayo alikuwa sehemu ya mpango mkubwa wa mashambulizi.
Obama alieleza kwamba, shambulio hilo lilisukumwa na msimamo binafsi wa mshambuliaji huyo na hakuna ushahidi kuwa, Marteen alipata maelekezo kutoka nje ya nchi kutekeleza mauaji.
Lakini, Mkurugenzi wa shirika la kijasusi la FBI,James Comey, alisema kuna ishara kuwa Marteen alishawishika kupitia mitandao ya intaneti ila bado haijajulikana kama kijana huyo alikuwa anaunga mkono kundi gani la kigaidi.
Comey alisema, muuaji huyo alieleza kuunga mkono kundi la wanamgambo wa Dola ya Kiislamu (IS) pamoja na kundi hasimu na IS la Al Nusra kutoka nchini Syria.
Katika hatua nyingine,Silaha mbili zilizotumiwa na Marteen zimebainika kununuliwa kwenye kituo cha kuuza silaha.
Mmiliki wa duka hilo Edward Henson, alisema Marteen alipitia taratibu zote zinazopaswa kufuatwa wakati wa kununua silaha hizo.
Naye mke wa zamani wa Marteen, Sitora Yusufi y, amemwelezea mumewe kama mtu aliyekuwa na tabia za ugomvi ya kutaka kupiga watu lakini hakuwa na itikadi kali za kidini.
Tukio hilo lililohusisha mauaji ya watu 50 na kujeruhi wengine zaidi ya 53 yalitekea kwenye klabu ya starehe ya mashoga iliyopo Frolida Jumapili ya wiki iliyopita.
Marteen,alivamia kwenye klabu hiyo kisha kuwafyatulia risasi mfululizo watu waliokuwepo ndani.
Wakati akitekeleza mauaji hayo, Marteen aliwateka nyara watu wengine zaidi ya 30 ambao waliokolewa na polisi.
Mtuhumiwa huyo ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi na polisi, ilielezwa alishawahi kuhojiwa na maofisa usalama mwaka 2013 na 2014 akihusishwa na makundi ya kigaidi.
Post a Comment