Waziri Nchemba Awafuta Kazi Viongozi Wote wa Wakulima wa Miwa Kuanzia ngazi ya Wilaya hadi Taifa
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. Mwigulu Nchemba akipewa maelekezo na mtafiti wa mbegu kutoka mmoja ya maafisa wa juu wa wakala mkuu wa ghala la mbegu za ASA (Agricultural Seed Agency) Mkoani Morogoro.
Mhe. Mwigulu Nchemba akikagua mbegu zilizopo kwenye ghala la ASA mkoani Morogoro.
Mwigulu Nchemba akizungumza na watumishi wa ASA (Agricultural Seeds Agency) wakati wa ziara hiyo. Kubwa alilosisitiza ni uzalendo na kufanya kazi kwa kujituma.
Mhe. Mwigulu Nchemba akipewa maelekezo kuhusu malisho ya ng'ombe yanayopatikana kwenye kituo cha utafiti wa mifugo Morogoro(LITA).
Mhe. Waziri akiangalia baadhi ya ndama wa ng'ombe waliopo kwenye shamba la utafiti kwenye kituo cha LITA - Morogoro.
Katika kikao hicho, wataalam kutoka SUA walisisitiza kuwa ili Tanzania iweze kuondokana na kilimo holela,ni wakati muafaka sasa kama nchi kuamua kuwekeza kwenye kilimo cha umwagiliaji na kuondoakana na kilimo cha mvua,pia kuachana na jembe la mkono na wakati huo huo kuimarisha vituo vya utafiti na kuzalisha mbegu kikanda.
Mhe. Mwigulu Nchemba akizungumza na Makamu Mkuu wa chuo za SUA(Sokoine University of Agriculture) alipofika kwaajili ya kukutana na wataalam,na uongozi wa SUA kwaajili ya kupokea maoni yao kuelekea kilimo,ufugaji na uvuvi wa kisasa. "Transformation of Agriculture".
Katika kikao hicho, wataalam kutoka SUA walisisitiza kuwa ili Tanzania iweze kuondokana na kilimo holela,ni wakati muafaka sasa kama nchi kuamua kuwekeza kwenye kilimo cha umwagiliaji na kuondoakana na kilimo cha mvua,pia kuachana na jembe la mkono na wakati huo huo kuimarisha vituo vya utafiti na kuzalisha mbegu kikanda.
Akiwa njiani kuelekea Ifakara, Mwigulu Nchemba akaamua kufanya mkutao Jimbo la Mikumi kijiji cha Tungu kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi dhidi ya uongozi wa miwa wilaya, Mkoa na Taifa, mahusiano mabaya ya kibiashara kati ya wakulima wa miwana kiwanda cha Ilovo na utitiri wa vyama vya wakulima kwa eneo la Kilombero.
Baada ya kusikiliza kero kutoka kwa wananchi na kusoma baadhi ya ripoti za serikali ya wilaya na mkoa na zile za tume mbalimbali zilizoundaw kujua kiini cha matatizo ya wakulima wa miwa Kilombero, Mwigulu Nchemba akiwa ndiye Waziri mwenye dhamana na kilimoakaamua kufuta uongozi wote kwa wakulima wa miwa kuanzia ngazi ya Wilaya ya Mikumi hadi Taifa kwa kosa la ubadhilifu na matumizi mabaya ya madaraka.
Mwigulu Nchemba akiteta jambo na Mbunge wa Mikumi Mhe. Joseph Haule (Prof. Jay) wakati wa mkutano huo
Mhe. Mwigulu Nchemba akiangalia mfereji ulioandaliwa kwaajili ya kusambaza maji kwenye shamba la utafiti wa mbegu za Mpunga-Kilombero. Matumizi ya mifereji kwenye kilimo yanaondoa mfumo wa kutegemea mvua ili mimea kupata maji na kukua kwa wakati.
Mwigulu Nchemba anatarajia kuendelea na ziara ya kukagua vituo vya utafiti na uzalishaji wa mbegu nchi nzima, lakini wakati huo huo atatembelea mashamba ya mifugo na maeneo ya uvuvi wa samaki.
Mwigulu Nchemba anatarajia kuendelea na ziara ya kukagua vituo vya utafiti na uzalishaji wa mbegu nchi nzima, lakini wakati huo huo atatembelea mashamba ya mifugo na maeneo ya uvuvi wa samaki.
Post a Comment