Header Ads

Viongozi wa Chadema Waanza Kuwasili Jijini Mwanza


Viongozi wa ngazi ya juu wa Chadema wameanza kuwasili jijini Mwanza ikiwa ni siku moja kabla ya kufanyika vikao vya juu vya chama hicho.

Leo, wajumbe wa Kamati Kuu wakiongozwa na Mwenyekiti, Freeman Mbowe watawasili jijini Mwanza.

Taarifa iliyotolewa jana na Mkuu wa Idara ya Habari wa Chadema, Tumaini Makene ilieleza kuwa Kaimu Katibu Mkuu, Salum Mwalim ameshawasili  na Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika na wakurugenzi wengine walitegemewa kuwasili muda wowote kwa ajili ya kikao cha Sekretarieti inayokutana kabla ya kile cha Kamati Kuu inayoketi kwa siku mbili kuanzia leo.

Baada ya kuwasili jijini Mwanza, Mwalimu alikutana na waratibu wa kanda zote za chama hicho ambako alipokea taarifa fupi ya maandalizi ya awali ya vikao vya Sekretarieti, Kamati Kuu na Baraza Kuu ambalo litaketi Machi 12 kisha kufuatiwa na kikao kingine cha Kamati Kuu Machi 13 asubuhi na jioni kutakuwa na mkutano mkubwa wa hadhara katika Viwanja vya Furahisha.

Machi 14, sekretarieti itakutana tena kuhitimisha vikao hivyo. 

No comments