VIDEO:Wachimbaji Wadogo Watano Wafariki Baada ya Kufunikwa na Kifusi
Kutoka Geita Info;
Wachimbaji wadogo Watano wafariki dunia na watatu kujeruhiwa baada ya kuangukiwa na kifusi cha mchanga wakati wakiwa katika harakati za kutafuta dhahabu katika kijiji cha Mgusu Mjini Geita.
Tukio hilo limetokea machi 9 majira ya saa kumi jioni ambapo baadhi ya wachimbaji waliingia katika eneo lilolozuiliwa kuchimba kutokana na eneo hilo kuwa hatarishi ambapo baada ya kuingia na kuendelea na uchimbaji ndipo kifusi kikaanguka.
Post a Comment