Header Ads

Rais Magufuli Awataka Wakuu wa Mikoa Kuwaweka Ndani Hata Masaa 48 Viongozi Wanaonyanyasa Wananchi


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Magufuli akihutubia Wakuu wa Mikoa wapya 26 na Watumishi wengine wa Serikali walioapishwa leo amesema; "Nimewateua ninyi (Wakuu wa Mikoa) muende mkawatumikie Wananchi na sio kwenda kufanya siasa. 

"Ilinichukua muda sana kuteua kwa sababu nilitaka kujihakikishia kuwa ninateua watu makini.

"Mkienda Mikoani nataka  mkatatue kero za Elimu, Ajira, Ujambazi na nyingine kwa kushirikiana na viongozi wengine na Mumtangulize Mungu naye atawasaidia.

"Kuna viongozi huko wananyanyasa wananchi, unakuta katibu tarafa, mtendaji wa kata ananyanyasa  tu  wananchi  bila  sababu.

"Ninyi  mna mamlaka  ya  kumuweka  mtu  ndani  hata  masaa 48. Kawawekeni wengi ili kusudi wajue kwamba wananchi wanatakiwa kuheshimiwa." Amesema Rais


==> Tazaidi, tazama  video  hii  kumsikiliza  Rais akiongea


No comments