Header Ads

Kiwanda cha Vipodozi Feki chanaswa Kigamboni Dar

Mamlaka ya chakula na dawa nchini Tanzania TFDA imebaini kuwepo kwa kiwanda bubu kinachozalisha bidhaa za vipodozi nchini Tanzania zenye lebo ya SAME inayoonesha kutengenezwa nchini Uturuki kinyume na sheria na taratibu za kuanzisha kiwanda na bila kukaguliwa na mamlaka hiyo kama ni salama kwa matumizi ya binaadamu.

Akiongea hii leo mkurugenzi wa TFDA Hiti Silo amesema kuwa awali walikamata shehena ya chupa 5,350 za pafyumu zenye thamani ya shilingi milioni 107 na walipomuuliza mmiliki wa duka hilo Dr Mohamed Gwao akasema bidhaa hizo zimeagizwa toka nchini Uturuki lakini walipofuatilia wakagundua zinazalishwa hapa nchini maeneo ya Mbagala Tuangoma

Aidha mamlaka hiyo ilipotembelea eneo hilo ilibaini mitambo mikubwa ya kuzalisha pafyumu hizo na kuchukua vifaa vyote kwa ajili ya kuvifanyia uchunguzi zaidi na watuhumiwa wamefikishwa kituo cha polisi.

Mamlaka ya chakula na dawa nchini inawatahadharisha watumiaji wote wa pafyumu hizo kuacha kutumia mara moja kwani bidhaa hizo hazijasajiliwa na TFDA na hivyo ubora na usalama wake haufahamiki.

No comments