DK.KALEMANI AACHA MASWALI BUKOMBE.
Naibu waziri wa Nishati na madini Dkt Medard Kaleman
NA MAKUNGA MAKUNGA.,
BUKOMBE.
NAIBU Waziri wa Nishati na Madini Dkt Medard Kalemani amewaacha
waanchi Wilayani Bukombe wakinung’unika baada ya kushindwa kujibu
maswali matano waliyomuuliza kwenye mkutano wa hadhara aliofanya
katika mji mdogo wa Uyovu –Runzewe akiwa na Mbunge wa jimbo hilo Doto
Biteko.
Dkt Kalemani aliuulizwa maswali hayo na wananchi ili awape majibu kwa
kumueleza kuwa “kwanini mnatugeuza kuwa watani wenu,wakati wa kampeni
mlituambia mtatupa maeneo ya kuchimba dhahabu lakini kila kukicha
mnakuja na walawala eti mchakato bado unaendelea, ,mara tuunde vikundi
,navyo tumeunda je mnataka hadi vikundi vingapi? Na tumeunda vikundi
hatupewi Leseni na tukienda mgodini tunapigwa tunaomba msitugeuze
watani wenu ipo siku mtakuja kuumbuka”Paul Kamula,said Juma na Mtoro
Melisy waliuliza.
Wananchi hao walidai kuwa wao wanataka wapewe majibu ya kuwa ni lini
wanaanza kuchimba Dhahabu kwenye maeneo waliotengewa si kupewa maneno
ambayo wameyasikiliza tangu wakati wa kampeni na baada ya kampeni
Mbunge wao amekuwa akifanya mikutano wimbo wake ni huohuo na baada ya
kumuona naibu Waziri wa madini wakadhani anayo majibu kumbe hata yeye
anawaletea propaganda.
Aidha wakamtaka Mbuge wao Doto Biteko aache tabia ya kuwapelekea
Mawaziri ambao hawana majibu sahihi ya kutatua changamoto na tatizo
waliyonayo ikiwemo la kuhitaji maeneo ya kuchimba madini ya Dhahabu vinginevyo
watakuja kuwazomea,wamesema.
Wamesema Rais John P.Magufuli amesema HAPA NI KAZI TU kwanini sasa
mawaziri na Mbunge anataka kuwachezea waache kuwachezea kwani maisha
yao ni kazi na kazi yao kubwa ni uchimbaji wa madini ambao umekuwa na
changamoto nyingi na vikwazo kutokana na kutokuthaminiwa wananchi
wanyonge na kukabidhiwa wawekezaji maeneo ambayo wameyahodhi na
hawayafanyii kazi. Wamemuomba Rais JPM awasikilize kilio chao na
kumuomba awaeleze Mawaziri wake waache kuwaalika kwenye mikutano ya
Propaganda watakuja aibika.
Naibu Waziri Dkt Medard Kalemani alihutubia mkutano wa hadhara mjini
Uyovu maarufu Runzewe kwenye viwanja vya mpira kwa mwaliko wa Mbunge
Doto ili awape majibu yatakayokidhi kiu yao wananchi lakini majibu
aliyoyatoa yameacha gumzo kubwa na manung’uniko katika mji wa
Runzewe,uyovu na Wilaya nzima kwani wananchi wa Bukombe maisha yao
yanategemea machimbo na shughuli mbalimbali zinazofanyika katika
migodi.
Katika mkutano huo baada ya wananchi kutokulizika na majibu ya naibu
waziri walianza kuguna na kisha kusambaa hali ambayo ilimfanya Mbunge
Doto kuwaomba wananchi wasimvue nguo wavute subira na kusema kuwa mambo
mazuri hayahitaji haraka wasikilize majibu ya Serikali kuwa tatizo lao
wanalishughulikia na si muda mrefu kiu yao itaisha yuko pamoja nao.
Dkt Kalemani ,aliwaambia wananchi hao kuwa Serikali inalifanyia kazi swala la
wachimbaji wadogo kupata maeneo ,pia tatizo la umeme tayari mkandarasi
yuko kazini watasambaziwa nguzo katika mitaa yao hivyo wasiwe na shaka
kwani serikali hufanya mambo yake kwa kufuata taratibu na kanuni zake.

Post a Comment