Amuua Mwanafunzi Mwenzake kwa Kumkata na Wembe
Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari ya Mtwara Ufundi mkoani Mtwara, Tawfiq Hamisi (17), amefariki dunia baada ya kukatwa na kiwembe katika mkono wake wa kulia na mwanafunzi mwenzake Issac Yohana (16).
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, kamanda wa polisi mkoa wa Mtwara, Henry Mwaibambe, amesema kabla ya kifo hicho kulikuwa na ugomvi kati ya marehemu na mtuhumiwa ambaye ni Isaac anayedaiwa kuficha kiatu cha mwenzie ambapo baada ya mzozano akaamua kumkata na kiwembe mwenzie chini ya bega lake la kulia.
Ameongeza kuwa marehemu ni mwenyeji wa mkoa wa Tanga huku mtuhumiwa ni mwenyeji wa wiayani Newala mkoani Mtwara, na kwamba taratibu za kuusafirisha mwili wa marehemu kuupeleka kwao zinafanywa na uongozi wa shule, huku mtuhumiwa akishikiliwa na jeshi la polisi kwa upelelezi zaidi.
Mganga mfawidhi wa hospitali ya Ligula, Dkt. Mdoe Mhuza, amethibitisha kupokelewa kwa mwili wa marehemu majira ya saa 11 alfajiri na kudai kuwa bado uchunguzi zaidi unaendelea kwa ajili ya kuweza kubaini chanzo cha kifo chake.
Post a Comment