Header Ads

Rais Dk John Pombe Magufuli leo amelihutubia taifa kupitia Wazee wa Dar -es- salaam


Rais Dk John Pombe Magufuli leo amelihutubia taifa kupitia wa Wazee wa Dar e salaam ambapo ameainisha changamoto kadhaa zinazolikabili taifa na mikakati inayochukuliwa na Serikali ya awamu ya tano kuikabili.

Akizungumza na wazee hao wa Dar es salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini humo, Rais Dk John Pombe Magufuli amewahakikishia Watanzania kwamba Serikali ya awamu ya tano anayoingoza imejipanga vyema kuwatumikia na kukabili matatizo yao.

Katika hotuba yako hiyo iliyochukua takriban saa moja na kugusa maeneo yote muhimu, Rais ametahadharisha viongozi na wananchi wengine kuhusu ubadhirifu wa mali ya umma.

Aidha, Rais Dk John Pombe Magufuli amezungumzia kuhusu hali ya kisiasa visiwani Zanzibar ambapo amesema yeye kama Rais ni vigumu kuingilia maamuzi ya tume ya taifa uchaguzi Zanzibar ambayo ni huru.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Dar es saalam alizungumzia changamoto mbalimbali zinazoukabili mkoa wa Dar es salaa hususan katika utekelezaji wa agizo la utoaji wa elimu bure.

No comments