Header Ads

MWANAMKE AUAWA KIKATILI GEITA.


Bi,Esther Masangija  mwenye umri wa maiaka 30  mkazi wa mtaa wa Mwatulole kata ya Buhalahala mkoani Geita , ameuawa kwa kukatwa na mapanga sehemu mbali mbali za mwili wake, huku mume wake  ndele simon miaka 39 akijeruhiwa vibaya sehemu za mwili wake hali ambayo imepelekea kulazwa katika hospitali  teule ya rufaa mkoani hapa.
Esther , aliuwawa  baada ya kuvamiwa nyumbani kwake na watu wasiojulikana majira ya saa nane usiku wa kuamkia febuari 18, ambapo marehemu  ameacha mume na watoto 2 akiwemo wa mwezi 1.
wakizungumza na PAUL BAHEBE BLOG mashuhuda wamesema kuwa wavamizi waliotenda kitendo hicho walipitia dirishani na kuvunja kisha kuingia ndani na kufanikiwa kutekeleza unyama huo.
Viongozi wa serikali ya mtaa na kata Mathias Mlasa ambae ni mtendaji wa kata hiyo na diwani  wa kata hiyo Mussa Kabese pamoja na mwenyekiti Charles Fikiri wamelaani vikali mauaji hayo na kuahidi kuwa wote watakaobainika kuficha wahalifu watapambana nao, kwani vitendo hivyo havivumiliki.


Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoani hapa,  Isaac Msengi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kwamba taarifa za awali za chanzo cha mauaji hayo  ni mgogoro kati ya marehemu na mtu mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa na anashikiliwa na jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi.

Bonyeza link hapo chini kuwasikia mashuhuda pamoja na viongozi wa mtaa huo wakizungumza;
http://www.audiomack.com/song/paul-bahebe-fm/mauaji-geita

HABARI:JOEL MADUKA #Stormfm #Geita

No comments